|
Mkakati wa Kupambana na Maambukizi ya VVU 2008 - 2012 |
|
Tanzania iliandaa na inaendelea kuutekeleza Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI kutokana na ukweli kwamba janga la UKIMWI ni tishio kubwa kwa mikakati ya maendeleo inayofanywa na sekta zote na wakati mwingine linaathiri maendeleo yaliyofikiwa awali.
Athari za janga hili zinasababisha machungu kwa mtu mmojammoja, familia na hata jamii yote nchini. Hata hivyo, kuna dalili za matumaini, kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni kiwango cha maambukizi ya VVU kinapungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi nchini. Read more ...
|